DIAMOND AWAHUSIA MASHABIKI WAKE KUMUEPUKA DIAMOND FAKE KWENYE FACEBOOK
Msanii mkali toka kwenye kiwanda cha Bongo Flavour, Diamond Platnumz hivi karibuni ameamua kufunguka juu ya mtu moja ambaye anatumia jina la “Diamond Platnumz Swaqq” kwenye facebook na kujifanya ni Diamond kumbe siyo na kufanya mambo ambayo yapo kinyume na vitu anavyovifanya Diamond mwenyewe.
Kuhusiana na kukelwa na vitendo hivyo Diamond aliamua kufunguka hivi kama njia ya kuwahusia mashabiki wake wamuepuke Diamond huyo feki kwenye Facebook kwa kusema maneno haya:”Kiukweli nimevumilia sana hii tabia ila naona kama uzalendo umenishinda…mara kwa mara nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa wadau wangu mbalimbali kuwa nawajibu vibaya kwenye account yangu ya Facebook, Kucomment maneno machafu,Ku_upload picha chafu,Kuomba vocha,Kuomba pesa kwa njia ya Western union, M-pesa,Tigo Pesa na kadharika…kiukweli jambo hilo limekua likinisikitisha sana…hususan kupitia katika account hiyo chini yenye jina la “Diamond Platnumz Swaqq” pamoja na Account zingine nyingi zenye majina na picha zangu…. hivyo ningependa kuchkua fulsa hii kuwajuza Mashabiki na wadau wangu kua Account hiyo yenye jina la “Diamond Platnumz Swaqq” si ya kwangu ni ya mtu Fake ambae anatumia jina na picha zangu kuwachezea akili zenu….”
Hii ndio Account ya Diamond Fake kwenye Facebook:
No comments:
Post a Comment