RIHANNA,BRUNO MARS,JUSTIN BIEBER WATA PERFORM KATIKA VICTORIA’S SECRET FASHION SHOW
Ni moja kati ya vinjwa ambavyo kiukweli nimeona jinsi miaka inavyozidi kwenda ndiyo dzain kama wanazidi ku shine katika game la muziki hawa si wangine bali ninawazungumzia Rihanna,Bruno mars,Justin bieber. Kama unakumbuka vizuri mwaka jana katika stage ya Victoria Secret Fashion Show walipanda wasanii watatu ambao wote ni wana hip hop lakini walipiga bonge la show kali hawa si wengine nawazungumzia Kanye west,Jay Z na Nick minaj.Sasa mwaka huu bhana wasanii watakao panda katika stage ya Victoria Secret Fashion Show siku ya tarehe 4 desemba ni Rihanna,Justin bieber,Bruno mars.Hawa ndiyo wasanii watakao perfom mwaka huu katika Victoria Secret Fashion Show.
SASA ILE TIME YA KUINGIA KILA WILAYA NA KUTOA ZAWADI ZA T SHIRT NA TICKET ZA FIESTA SERENGETI IMEFIKA NA LEO IMEANZIA ILALA
Fundi mitambo akiweka mambo sawa kabisa ili wakazi wa Dar es Salaam waje maeneo ya mnazi mmoja ili wajishindie t shrt na ticket za fiesta serengeti.
Antu mandoza na George wa clouds tv bhassssssss
Ni moja kati ya vijana ambao walikuwa wakitoa burudani kwa wakazi ambao waliohudhuria katika maeneo ya mnazi mmoja kuja kujipatia t shirt na ticket za serengeti fiesta kwa njia ya maswali.
Wakazi wa wilaya ya ilala walikusanyika kwa pamoja katika viwanja vy mnazi mmoja leo kuja kujishindia t shirt na ticket za serengeti fiesta leo mchana Jijini Dar es Salaam.
Muli B akimkabidhi zawadi ya t shirt kwa mkazi wa wilaya ya ilala baada ya kujibu maswli yake kwa usahihi kabisa.
Shadee kutoka clouds television akiongea na wakazi wa ilala kuhusu msimu huu wa Serengeti Fiesta wanampokeaje mtu mzima Rozay dzain kila mmoja ukimuona hapo jinsi anavyotiririkaa.
Adamu mchomvu a.k.a Baba john yeye aliamua kuja na style yake ya kuuza pipi,sigara katika viwanja Mnazi mmoja leo Jijini Dar es Salaam.
Baba john akimpa mteja sigara baada ya kununua kwake duuuhh kweli huu ni muonekano mpya na burudani kibao.
Ni moja kati ya wakazi wa ilala wamejishindia zawadi ya t shirt na ticket ya serengeti fiesta.
Antu Mandoza akikabidhi zawadi kwa mkazi wa ilala ambaye amejishindia tshirt pamoja na Ticket ya Serengeti Fiesta baada ya kujibu maswali jinsi yalivyokuwa yanaitajika kujibiwa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Kama unavyoona zoezi linaendelea la kugawa T shirt na ticket za Serengeti Fiesta.
Burudani mbalimbai ziliweza kutolewa kwa wakazi wa mnazi mmoja.
T.I.D NDANI YA SERENGETI FIESTA
Kama unakumbuka kipindi cha nyuma msanii huyu aliamua ku post katika ukurasa wake wa facebook na kulalamika kwamba huu ni mwaka wake wa 5 ajapewa hata nafasi ya kupiga show za fiesta.Sasa habari nzuri ni kwamba msanii huyu anayefahamika kwa jina la Mnyama au TID atakuwa ni moja kati ya wasanii ambao wataonyesha muonekano mpya na zile burudani kali katika stage ya Serengeti Fiesta.
DIAMOND PLATNUM AINGIA MKATABA NA I-VIEW MEDIA
Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na Msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.
Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto) na msanii Diamond Platnumz wakisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja.Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.
BOW WOW AMEKUWA HOST MPYA NDANI YA BET "106 AND PARK"
Ni moja kati ya wasanii wanaotokea zile pande za state huyu si mwingine anajulikana kwa jina la Shad Gregory Moss katika upande wa muziki anafahamika kwa jina la Bow wow.Sasa basi habari nzuri ni kwamba msanii huyu ametangazwa rasmi kuanzia sasa atakuwa host mpya katika kipindi cha "106 & Park" kinachorushwa katika station ya Black Entertainment Television.Kwa hiyo msanii huyu atakuwa one of four new hosts for the TV show,which recently entered its twelfth year on the air.Kwa hiyo mashabiki wa Bow wow dzain kama inawahusuuu hii.









Post a Comment