NAOMPENDA JOKATE MWEGELO, HII NDIO HABARI ALIYOITANGAZA LEO MCHANA.
Posted: 10th October 2012 by MillardAyo in News
Mrembo Jokate Mwegelo baada ya watanzania wengi kumfahamu kwa kujihusisha na ishu za urembo, leo mchana ametangaza goodnews kwa kuzindua kampuni yake ya KIDOTI ambapo pia bidhaa yake mpya ya nywele imezinduliwa.
Ni kampuni ambayo haikua rahisi yeye kuianzisha kutokana na kukatishwa tamaa, alitamani kuwa na hii kampuni toka miaka minne iliyopita lakini mwaka jana ndio akapata mtu wa kumsaidia kutengeneza hizo bidhaa ambazo mtaji wake ni zaidi ya dola za kimarekani elfu thelathini ambazo ni zaidi ya milioni 40 za Tanzania.
Kabla ya kuanza kuzitengeneza hizi nywele, Jokate ambae ana masters ya mambo ya siasa alifanya utafiti wa hiyo biashara kwa karibu mwaka mzima, na sasa zitakua zinauzwa kwenye saluni mbalimbali za kike Tanzania.
Hizi nywele zinatengenezwa hapahapa Tanzania ambapo J amesema sehemu ya faida yake ataitumia kusaidia wasichana wa Ruvuma ambapo timu nzima ya kampuni ya Kidoti ni watu sita.
Jokate atasikika kwenye AMPLIFAYA ya Clouds Fm kuanzia saa moja usiku leo october
Post a Comment