Adsense

Binamu wa Diamond kuiwakilisha Tz BBA 2013?

.
.
Wiki iliyopita hii ndio iliingia kwenye Top 10 ya AMPLIFAYA Clouds FM kama stori iliyozungumziwa na Watanzania sana kwa wiki nzima sehemu mbalimbali kuanzia mitaani mpaka kwenye mitandao ya kijamii.
Rommy Jones alipopata nafasi ya kuongea kwenye exclusive interview na millardayo.com amesema ni kweli hizo stori zimekuepo lakini yeye mwenyewe hana uhakika kama atashinda kwenda BBA 2013 na mpaka sasa hajajua kitakachotokea.
“kushiriki nilishiriki ila sina uhakika manake sijapigiwa simu na Multichoice wala BBA kuhusu mimi kushinda, napenda kwenda…. ikitokea nimekwenda nitafurahi manake ni hela zile pia” – Rommy
Rommy ambae ameshiriki usahili wa BBA kwa mara ya kwanza mwaka huu, amewahi kufanya kazi Clouds Tv lakini pia ukaribu wake na mastaa mbalimbali wa Tanzania umemfanya kujulikana kwenye kona kibao ndani ya ardhi ya JK.
Taarifa zilizosambaa kuanzia wiki iliyopita zimeamplfy kwamba Rommy alikwenda South Afrika siku kadhaa zilizopita kwa ajili ya usahili mwingine wa mwisho kabla ya kuingia BBA huku stori nyingine pia zikimtaja msanii wa kike ambae jina lake linaanza na herufi F, kwamba na yeye anaiwakilisha Tanzania mwaka huu.
Pamoja na kwamba hizi ndio stori zinazozungumzwa sana na baadhi ya Watanzania, bado hakuna uhakika kama kweli hawa ndio wanaiwakilisha Tanzania.. tusubirie siku yenyewe
.
Rommy kwenye interview na host wa Amplifaya na Top 20 za Clouds FM, Millard Ayo
.
.
.
.
.
Rommy Jones akiwa na Diamond toka utotoni mpaka hapa walipo
Kwa mujibu wa afisa uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, ni zaidi ya watu 100 waliojitokeza kwenye usahili ambapo watu maarufu ni zaidi ya watano.
Mshindi wa BBA 2013 atachukua USD 300000.

No comments