APPLE WASHINDWA RUFAA YA KESI DHIDI YA SAMSUNG
LONDON-UINGEREZA,
Mahakama ya rufaa nchini Uingereza imeipa ushindi kampuni ya Samsung ya Korea dhidi ya mahasimu wao kampuni ya Apple ya nchini Marekani.Katika kesi hiyo ambayo Apple wanailalamikia Samsung kwa kutengeneza simu za Samsung Galaxy zenye muundo unaofanana na wa simu zao za Iphone walikuwa wakitaka kusimamishwa kwa uuzwaji wa simu hizo barani Ulaya.
Katika maamuzi hayo mahakama imekiri kuwa simu za Samsung zinafanana na zile za Apple lakini ikaongeza kuwa hazina uhusiano na uigaji wa aina yoyote kutoka kwa simu za Apple, pamoja na maamuzi hayo mahakama imeitaka kampuni ya Apple kutangaza katika tovuti yake na baadhi ya magazeti yatakayoamriwa kuwa Samsung hawakunakili muundo wao.
Kampuni ya Apple imekataa kuongelea chochote juu ya suala hilo huku Samsung wakisema wamepokea kwa furaha uamuzi huo.

Post a Comment