UKUTA WA ELIMU NA MAISHA KATI YA WALICHONACHO NACHO NA WASICHO NACHO LINI UTAVUNJWA?
Watoto
Angela mwanafunzi wa darasa la 5 na Michael mwanafunzi wa darasa la 6
wote wanafunzi wa shule ya msingi Sinde jijini Mbeya, Kamera ya Chimbuko
Letu ilishuhudia wakimwagilia mboga mboga wakati wa weekend ili waweze
kupata fedha za kujinunulia mahitaji madogomadogo ya shuleni.
Jiji la Mbeya likionekana kupendeza huku barabara zikihimarishwa kwa usafi mkubwa
Wakati
mazingira ya Jiji yakionekana kuwa mazuri katika hebu tazama mama huyo
ambaye anaishi kata ya Sinde mtaa wa Kijani Bichi Ilolo akiishi kwenye
nyumba hii je kuna usawa kweli wa maisha na kipato?
Mtoto Michael akimwagilia Mbogamboga
Mtoto Angela akimwagilia kiunga chake cha Mboga mboga mara baada ya mapumziko ya shuleni Chimbuko Letu ilishuhudia kwa ukaribu.
Watoto hao ndugu wakishirikiana kumwagilia Mboga katika maeneo ya Ilolo Jijini Mbeya Chimbuko Letu ilishuhudia kwa ukaribu.
Watoto
wakazi wa kata ya Sinde Mtaa wa Kijani Bichi Ilolo wakitumikishwa
kubeba matofali kwa ujira wa shilingi 10 kwa kila tofali Chimbuko Letu ilishuhudia kwa ukaribu.
Viongozi na wanaharakati ajira za watoto zitakomeshwa na nani?Je elimu kwa wanawake itawezekana kwa hali hii.?
Kwa hali hii mtoto akianza mapema kutafuta pesa kuna elimu ya baadae kweli, Haki iko wapi basi ndugu zangu?
WAZAZI TUNAFUATILIA TABIA NA SEHEMU ZA WATOTO WETU WANAZOZITUMIA KUCHEZEA KWELI Chimbuko Letu ilishuhudia kwa ukaribu.
MAJI HAYA YANAFAA KWA MTOTO KUOGA?
SEHEMU HII KWELI SAMAKI ANAWEZA KUPATIKANA AMA VYURA VINAWEZA KUPATIKANA
Ajira na utumikishwaji watoto namna hii katika kata ya Isanga nani wa kuukomesha?
NANI ALAUMIWA KWA UCHAFU WA MAZINGIRA, SERIKALI AU WANANCHI?
Kwa hali hii kunamtu atakayepona kweli, TUOMBE MUNGU ATUNUSURU DHIDI YA MAGONJWA.
Kijana
huyo akitoka kuchota maji kwenye Mto Jihanga kutokana na tatizo la
maji linaloendelea kulikumba Jiji la Mbeya baada ya mabomba mengi
kukatwa wakati wa ukarabati wa barabara.Chimbuko Letu ilishuhudia kwa ukaribu.
Si
vibaya kwa mtu akifariji kuwa anamiliki gari, kama hapa unapomuona
mezee huyu mkazi wa Mwanjelwa mtaa wa Makunguru kata ya Ruanda akijipa
faraja kwenye gari lililo juu ya mawe huku akipewa faraja na jirani
yake.
PICHA ZOTE NA CHIMBUKO LETU BLOG
PICHA ZOTE NA CHIMBUKO LETU BLOG
Post a Comment